Jumatano , 7th Oct , 2015

Kampeni za wagombea Urais wa Tanzania kupita vyama tofauti wameendelea tena jana huku vyama vitatu vikiendelea kushambulia kanda ya kaskazini na kuendelea kumwaga sera zao kwa wananchi wa maeneo hayo.

Wagombea Urais kupita Act-Wazalendo,CHADEMA, na CCM, wakihutubia mikutano tifauti ya Kampeni

Akihutubia mikutano ya hadhara kwa nyakati tofauti katika jiji la Arusha katika wilaya ya Monduli na Arusha Mjini Mgombea urais kuptia chama cha mapinduzi Dkt. John Magufuli ameahidi kufanyakazi mfano wa Waziri mkuu wa Zamani Marehem Edward Moringe Sokoine.

Naye mgombea urais anaeungwa mkono na UKAWA kupita CHADEMA Mh. Edward Ngoyai Lowassa akihutubia katika mikutano tofauti katika wilaya za Same na Mwanga aliahidi kulishughulika tatizo la umeme ambalo kwa sasa limekuwa kero kwa wananchi.

Kwa upande wake mgombea urais kupitia chama cha ACT-Wazalendo Mama Anna Mghwira akiwa wilayani Arumeru mkoani Arusha aliahidi kudumisha mafao ya wafanyakazi ili kila mtanzania awe na maisha bora baada ya kustaafu katika shughuli zake.