Jumatatu , 16th Jun , 2014

Uongozi wa Halmashauri Mkoani Mwanza umetakiwa kuwaondoa mapema wafanyabiashara wadogo wanaopanga biashara sehemu zisizoruhusiwa kabla hakujatokea athari.

Baadhi ya wafanyabiashara mkoani Mwanza wakiwa wamebeba bango wakati wa vurugu za wafanyabiashara hao hivi karibuni.

Katibu uenezi wa CCM Mkoani Mwanza, Simon Mngelepa alisema kutowaeleza mapema wafanyabiashara hao ndiyo husababisha vurugu kama zilizotokea awali kati ya polisi na wafanyabishara hao.

Aidha wafanyabishara hao ndogondogo walitakiwa kufuata sheria na taratibu za halmashauri za kufanya biashara kwenye maeneo yanayoruhusiwa ili kuepusha malumbano yasiyo na tija.