Jumamosi , 14th Mei , 2022

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete ameonya kuwa hatopenda kusikia malalamiko kutoka kwa mwananchi ambaye tayari amekamilisha taratibu za kumilikishwa   ardhi analalamikia ucheleweshaji wa hati na kuwataka maofisa wa ardhi kuwa waadilifu ili kutenda haki k

‘’Wale wote ambao wametoa anuani zao ni maelekezo yangu kwamba muwafikie wako vijana ambao wanafanya kazi ndani ya Mbeya muwatumie kuharakisha na kama hawatoshi fedha zipo za kuongeza nguvu kazi hiyo.’’ Alisema Ridhiwani.

Naibu Waziri ameongeza kuwa pia hatarajii uzembe wa aina yoyote kwani Wizara yake inaajiri vijana wapya ili waje kuongeza nguvu katika zoezi zima la kupanga, kupima na kumilikisha ardhi.

Naibu Waziri Kikwete alisema hayo tarehe 13 Mei Mwaka huu wakati wa zoezi la ugawaji hati na leseni za makazi kwa kata 14 na 

Mitaa 67 ambapo mradi wa utambuzi vipande na utoaji lesseni za makazi umefanyika kwenye Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

‘’Tunaposema ardhi hii ina thamani kiasi gani ni razima iwe imepimwa lakini kama una heka kumi ambazo hazijapimwa thamani ya ardhi hiyo ni sifuri.’’Aliongeza Ridhiwani Kikwete Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Aidha Kikwete amemtaka Kamishna wa Ardhi Mbeya kuomba fedha zaidi kwa mwaka wa fedha ujao ili kuhakikisha maeneo ambayo hayajafikiwa na mradi wa kupanga, kupima na kumilikisha ardhi   apimiwe ardhi yake na kupata hati.

Naibu Waziri aliongeza kuwa kwa mwaka wa fedha hujao Wizara yake natarajia kupata fedha takribani Bil. 345 kwa ajili ya kuendelea na miradi ya upimaji ardhi hivyo kuwataka Mbeya kuomba fedha ili kuwezesha kupima ardhi kwa wananchi.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete amesema kwa wananchi kupewa hati ya kipande cha ardhi ni ukombozi tosha kiuchumi kwani hati hiyo inakuwa dhamana ya mwananchi katika kupata mikopo ikiwemo kutambua mipaka ya ardhi yake na ongezeko la thamani ya ardhi.  

Akizungumza baada ya kupatiwa hati yake Chifu Roketi Mwashinga amesema kuwa baada ya kupatiwa hati yake sasa anaamini kuwa anamiliki nyumba tofauti na awali ambapo alizoea kusikia watu wengine wakisema kuna nyumba zilizopimwa ambazo waliishi watu kadhaa.

‘’Zamani nyumba zetu zikuwa zinaitwa kota lakini sasa baada ya kupewa hati sasa jina hilo litakoma na kuitwa Nyumba kutokana na ardhi yake kurasimishwa rasmi’’. Aliongeza Chifu Mwashinga.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaendelea na zoezi la Kupanga, Kupima na Kumilikisha ardhi katika Mikoa mbalimbali na kwa mkoa wa Mbeya vipande 11,880 vimetambuliwa katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya.