Alhamisi , 30th Mar , 2023

Walinzi wanane na maafisa kadhaa wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji kufuatia moto uliozuka kwenye kituo cha wahamiaji kaskazini mwa mji wa Ciudad Juarez nchini Mexico na kuua wahamiaji 39.

 

Mwendesha mashtaka katika masuala ya haki za binadamu Sara Irene Herrerias amesema uchunguzi unafanyika juu ya tuhuma za mauaji na uharibifu wa mali.

Uchunguzi unaendelea juu ya wanaume watatu waliovaa sare walioonekana kwenye video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii wakishuhudia tukio hilo bila kuchukua hatua yoyote wakati moto ukiendelea kuwaka. 

Awali Rais wa Mexico Andrés Manuel López Obrador, alitaja chanzo cha moto huo kuwa ni wahamiaji waliochoma moto magodoro baada ya kusikia watarejeshwa kwenye mataifa yao.