Jumanne , 4th Oct , 2022

Msemaji wa Idara ya Uhamiaji nchini Paul Mselle, amesema kwamba endapo mtu atazingatia taratibu zote za uombaji wa hati ya kusafiria (Passport), anaweza kuipata ndani ya siku moja hadi siku saba za kazi.

Passport

Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba 4, 2022, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio.

"Mtu akikamilisha taratibu zote vizuri za uombaji wa passport kuipata kwake inaweza kuchukua siku moja mpaka siku 7 za kazi, kuna wengine wanakuja wana dharura hata ndani ya siku moja anaweza kupata," amesema Mselle