Jumanne , 15th Dec , 2015

JESHI la polisi mkoani Njombe linawashililia Wahabeshi 29 kutoka Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini bila kibali pamoja na madereva wao 3 raia wa kitanzania maeneo ya Makambako mkoani humo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Wilbroad Mtafungwa

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Wilbroad Mtafungwa alisema kuwa watu hao waliokamatwa ni wahabaeshi kutoka Ethiopia walikuwa wakeelekea mpaka wa Tanzania na Zambia ili waelekee nchini Afrika Kusini walikamatwa maeneo ya Makambako mkoani Njombe Juzi majira ya saa Usiku baada ya gari yao moja kuharibika ambapo walikuwa na magari mawili.

Amesema kuwa baada ya kufika katika gari hizo aina ya Toyota Haice zenye namba za usajili T 998 BGZ na ya pili Totota haice super Costumer yenye namba za usajili T 371 DDR, na kuwa katika tukio hilo waliwakamata watu watatu walio kuwa wakisaidiana kuendesha magari hayo.

Amesema kuwa wahabeshi hao watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi wao wakishirikiana na idara ya uhamiaji ili sheria kuchukua mkondo wake.

Aliwataja madereva hao waliokuwa wakisaidiana kuwa ni Issa Alli, Noeli Yohana wote wakazi wa Mikomi mkoani Morogoro na Juma Zuberi Mkazi wa Dar es Salaam.

Amesema kuwa baada ya uchunguzi kukamilika watawafikisha pia mahakamani na kuwataka watanzania wawe makini na watu wa aina hiyo kutokana na duniani kuwa na wimbi kubwa la Ugaidi hivyo taarifa za kuwapo kwa watu wa aina hiyo kutoa taarifa ili kuwadhibiti kabla hawajaleta madhara.

Aidha mmoja wa madeva wa magari hayo Issa Ally amesema kuwa yeye hakuelewa kuwaaliowapakiza ni watu gani kutokanana yeye kuambiwa kuwa anawabeba watu wa harusi ambapo hakuweza kuwachunguza kutokana na kuwa ilikuwa ni usiku na mvua ilikuwa inanyesha.

Hata hivyo Mmoja wa wahabeshi hao amesema kuwa wanaelekea nchini Malawi ambako wameambiwa kuwa kunakazi wametoka nchini kwao kutokana na ugumu wa upatikanaji wa ajira.