Prof. Benno Ndulu amefariki dunia

Jumatatu , 22nd Feb , 2021

Aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu, amefariki dunia leo asubuhi.

Prof. Benno Ndulu

Profesa Benno Ndulu alikuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2018. 

Profesa Ndulu pia aliwahi kuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na pia aliwahi kufanya kazi Benki ya Dunia.