Rais Magufuli serikali haijakataza barakoa

Jumapili , 21st Feb , 2021

Rais Dk. John Magufuli amewataka Watanzania kuwa makini na barakoa wanazovaa kwani zipo nyingine ambazo sio salama huku akiweka wazi kuwa wachukue tahadhari zaidi ikiwemo kujifukiza kwani hata wasaidizi wake wameugua na wamepona.

Rais Dk. John Magufuli

Dk. Magufuli ameyasema hayo leo jumapili Februari 21, 2021 aliposhiriki katika Ibada ya Dominika ya Kwanza ya Kwaresima katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

“Sijasema msivae barakoa wala msininukuu vibaya, ila kuna barakoa nyingine sio nzuri, huu ndio ukweli, mimi ni kiongozi wenu najua mengi na lazima niwaambie ukweli,” alisema Rais Dk. Magufuli.

Ameongeza kuwa, ''Hebu tutaje nchi gani ambayo watu hawajafa na corona, maelfu wanakufa, kunanchi walipoteza watu 3000 kwa siku na wanavaa barakoa, sisi tuchukue tahadhari, wapo wasaidizi wangu wengine wameshaugua, watoto wangu wameshaugua, wadogo zangu wameshaugua na wameshapona''.

Zaidi tazama video hapo chini.