Jumatatu , 5th Dec , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagiza kiasi cha shilingi milioni 960 zilizotengwa kwaajili ya sherehe za maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru  wa Tanzania zitumike  katika ujenzi wa shule za wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika mikoa nane ya Tanzania bara

Taarifa iliyosomwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachane jijini Dodoma imeeleza kuwa mwaka huu hakutakuwa na gwaride maalumu la Uhuru