Sakata la Membe kuondoka ACT Wazalendo lazungumzwa

Jumatano , 24th Feb , 2021

Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, amesema kuwa aliyewahi kuwa mshauri wa chama hicho Bernard Membe, aliondoka ndani ya chama hicho kwa hiari yake mwenyewe na hakufukuzwa na mtu yeyote na kwamba kama atataka kurudi tena basi anakaribishwa.

Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje mstaafu, na aliyewahi kuwa mshauri wa Chama cha ACT Wazalendo

Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 24, 2021, kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, ambapo pia ametumia nafasi hiyo kuviomba vyama vingine vya siasa kuhakikisha vinatoa nafasi kwa wanachama wao ambao watakuwa wameiridhisha nao.

"Siasa ni 'dynamic' Bernard Membe tulimpokea na baadaye alijitoa ndani ya chama chetu, hatujutii kumpokea lakini tumejifunza mengi kutoka kwake, unajua kuna vitu vinakuwa ndani ya mtu huwezi kuviona kwa macho", amesema Dorothy.

"ACT Wazalendo tutaendelea kuwa kimbilio la watu wanaotaka kufanya siasa safi, siasa za maendeleo na matendo, Membe akirudi tena anayo haki ya kupokelewa hatukatai wanachama sisi hatukumfukuza aliondoka yeye mwenyewe", ameongeza.