Jumanne , 26th Jan , 2016

Serikali imezitaka kamati za maafa kuanzia ngazi ya kata mkoa na wilaya kushughulikia matatizo ya maafa ikiwemo mafuriko na ukame unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi ili kuokoa maisha ya kazi wa eneo husika.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama

Akijibu bungeni katika kipindi cha maswali na majibu kuhusu suala la serikali kuwasaidia waathirika wa mafuriko, Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama amesema serikali itasaidiana na kamati hizo pale utakapohitajika msaada zaidi kutokana na maafa hayo.

Bi. Jenista amesema kutokana na Mabadiliko ya Tabia nchi Tanzania ni moja kati ya nchi zilizoathirika na hali hiyo, hivyo ni vyema kamati za maafa zikafanya kazi kwa ukaribu na serikali ili wakisaidiana na wananchi wa maeneo yanayoathirika na hali hiyo.

Mhe. Jenista ametoa kauli hiyo baada ya mbunge wa viti maalum (CCM), Felista Bula aliyetaka kuja serikali ina mpango gani wa kudumu wa kuwasaidia waathirika wa mafuriko ambao mpaka sasa wengi hawana mahali pa kuishi pamoja na kukabiliwa na baa la njaa.