Jumatano , 9th Sep , 2015

Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Mh. John Pombe Magufuli amesema ni dhamira ya Serikali yake ya awamu ya tano kuifanya mwambao wa Bahari ya Hindi Tanga ikiwemo kuwa kuwaa ukanda wa Viwanda ili kuweza kutoa ajira hasa kwa vijana.

Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Mh. John Pombe Magufuli akihutbia wakazi wa Tanga

Akizungumza na Wananchi wa Jiji hilo waliojitokeza kusikiliza sera zake Mh. Magufuli amesema kuwa amedhamiria kujenga vipya na kuvifufua viwanda nchini lakini pia kuwanyang,anya wale wote waliopewa dhamana ya kuviendeleza viwanda na wakashindwa.

Aidha Magufuli ameongeza kuwa ataunda kikosi maalumu cha kushughulia ulinzi wa bahari ya hindi kwa kuwa kuna maharamia ambao wamefanya sehemu ya bahari iliyop eneo la Tanzania kama shamba la Bibi kwa kuvua samaki kinyume na Taratibu.

Wakati huo huo Mgombea Mwenza wa Chama cha Mapinduzi CCM, Bi. Samia Suluhu amewataka Wananchi hasa waishio vijijini hususani wanawake kujitokeza kwa siku ya kupiga kura October 25 na kupuuzia kauli za kuwa siku hiyo kutakuwa na Vurugu.

Akiongea katika mikutano ya Hadhara Wilaya ya Nyasa na Mbinga Mkoani Ruvuma Bi. Samia amesema kuwa kuna kauli zinatolewa na baadhi ya Watu ili kuwatisha wanawake wasijitokeza kupiga kura siku ya uchaguzi hivyo kutaka kuwanyima haki yao ya msingi.

Akiwa katika vijiji cha Kingeliti, na Tindi katika jimbo la Nyasa na kijiji cha Maguu katika Wilaya ya Mbinga aliwataka wananchi wa vijiji hivyo wapuuzie kauli za vitisho ya kuwa hawataweza kupiga na kuongeza kuwa serikali imejipanga vizuri ili kufanya uchaguzi wa huru na wa Haki.