Ijumaa , 1st Jul , 2022

Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023  imepanga kusimika mitambo 57 ya hewa tiba ya Oxjeni katika Hospitali zote za Rufaa za mikoa,Kanda pamoja na Hospitali za Wilaya nchini.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mara baada yakuzindua mtambo maalum wa uzalishaji hewa tiba ya Oxjeni katika Hospitali ya kibingwa ya Benjamin Mkapa uliogharimu Bilioni 1.5 ambapo amesema kituo hicho kitazalisha mitungi 400.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy ametangaza kuanzia leo tarehe 1 mwezi wa 7 mwaka 2022 serikali imesitisha rasmi matumizi ya fomu ya 2C katika Hospitali zote za umma zinazotumia bima ya afya mara baada yakuonekana kuna  udanganyifu mkubwa unafanyika.

Fomu ya 2C ni karatasi inayoandikwa dawa nakupatiwa mgonjwa akaitafute dawa hiyo nje ya Hospitali au vituo vingine tofauti na alipotibiwa mgonjwa.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dk. Alphonce Chandika amesema kabla yakufungwa mitambo hiyo kipindi cha mlipuko wa Uviko 19 ,Hospitali hiyo ilikua inatumia mitungu 200 kwa siku kwa kutumia gharama ya shilingi milioni 10 na ilikua ikifwatwa Dar es salaam kwakua wao hawakua na uwezo wakuzalisha hewa ya Oxjeni.