Jumatatu , 26th Oct , 2020

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, amesitisha minada na magulio yote mkoani humo siku ya uchaguzi mkuu ya Oktoba 28, 2020, ili kutoa nafasi kwa wananchi kwenda kupiga kura kumchagua Rais, wabunge na madiwani wanaowataka.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka.

RC Mtaka ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Maswa, na kusema kuwa minada na magulio yataendelea siku ya Alhamisi kama kawaida.

"Minada inayofanyika jumatatu na jumanne ni ruksa, Jumatano hakuna mnada, Oktoba 28, 2020, mnada hautafanyika ili Watanzania waliojiandikisha wapate nafasi ya kupiga kura", amesema RC Mtaka.

Kwa upande wake, msimamizi wa uchaguzi majimbo ya Maswa Magharibi na Maswa Mashariki mkoani Simiyu, Fredrick Saganiko, amewaapisha wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi watakaohudumu zaidi ya vituo 500 majimbo hayo, kisha akahimiza uchaguzi ufanyike kwa haki, utulivu na amani.