Ijumaa , 8th Jul , 2016

Watanzania wametakiwa kusomea fani zenye fursa pana ya soko la ajira ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa ajira ambalo linaendelea kuota mizizi kwa sasa nchini.

Mkurugenzi Mkazi wa Universites Abroad Link, Tony Rodgers Kabetha akifafanua jambo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa taasisi ya University Abroad Link, Tony Kabetha wakati wa utiaji saini wa mkataba wa ushirikia na chuo Kikuu cha Teknolojia cha Shenyang cha China.

Bw. Kabetha amesema kuwa wanafunzi wengi hawasomi kwa vitendo, wanashindwa kutambua kujiunga na fani ambazo zinaongoza katika kuzalisha ajira kama sekta ya gesi na mafuta.

Tanzania ni moja ya nchi yenye tatizo kubwa la ajira duniani ambapo inakadiriwa kuwa wahitimu zaidi ya milioni moja kila mwaka huku wenye uhakika wa ajira kwenye sekta rasmi hawazidi laki tatu kwa mwaka.

Bw. Kabetha amesema kuwa kumekuwepo na jitihada kubwa za serikali kuwekeza kwenye sekta ya elimu pamoja na kujenga mashule ili kukuza elimu lakini ajira bado ni changamoto kuwa kwa wananchi wa Tanzania.