Ijumaa , 5th Aug , 2022

Tanzania inaendelea kubainishwa kama nchi iliyo hatarini kukabiliwa na athari za mabadiliko tabia ya nchi inayotishia ukuaji wa uchumi na maendeleo endelevu huku suluhisho ikitajwa kuwa ni kutumia nishati mbadala ikiwa ni mfumo salama wa matumizi ya Nishati.

Ripoti ya Mipango endelevu ya Wentworth ya mwaka 2021 inaitaja Gesi asilia kama mbadala wa vyanzo vya nishati zinazochafua mazingira ikiwemo mafuta mazito na diseli ambayo itakuwa fursa ya kuiwezesha Tanzania kukua kiuchumi.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Wentworth Katherine Roe wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Ripoti ya Mipango endelevu ya Wentworth iliyofanyika jijini Dar es salaam inayoelezea mtazamo wa makakati endelevu unaowiana na malengo ya maendeleo endelevu SDGs ya kimataifa inayozingatia nguzo tano ikiwemo kuwezesha mabadiliko ya nishati na utawala dhabti wa mazingira,kijamii na utawala.

Kwa sasa mahitaji ya gesi nchini yanatumika kwa kiasi kikubwa kuzalisha umeme kwa asilimia 79 ikifuatiwa na mahitaji ya viwanda kwa asilimia 21 na kisha matumizi ya nyumbani na gesi asilia iliyosindikwa.

Kwa Mujibu wa taarifa yake amesema Gesi inayozalishwa na Mtambo wa kuzalisha gesi wa Mnazi bay iliopo katika Bonde la Ruvuma Kusini mwa Tanzania imechangia asilimia 50 ya mahitaji ya gesi asilia nchini ambapo hatua hiyo imesababisha lita bilioni 4.6 za dizeli na mafuta mazito kuacha kutumika kutokana na matumizi ya gesi asilia