Jumatatu , 11th Apr , 2016

Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani balozi Hassan Simba, amesema serikali ya Tanzania na ya Uganda, zipo katika mkakati wa pamoja wa matumizi ya rasilimali zinazopatikana katika mipaka ya nchi hizo mbili.

Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani balozi Hassan Simba.

Balozi Simba ameyasema hayo wakati akiongoza ujumbe wa Tanzania,katika mkutano wa kuidhinisha ripoti ya upimaji na uhakiki wa mipaka baina ya Tanzania na Uganda kazi iliyofanyika mwaka 2003.

Balozi Simba amesema maeneo mengi ya mipakani yana maeneo ya uzalishaji ambapo wanaweza kuzalisha Nishati ya Umeme kwa kutumia maji ambapo inaweza ikazinufaisha nchi zote mbili.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mkutano huo wamesema kuwa watu wengi wa mpakani hawajui taratibu zakuvuka mipaka hivyo kusababisha migogoro midogomidogo baina ya wakazi wa maeneo hayo.

Wajumbe kutoka nchi hizo mbili wanatarajiwa kutembelea maeneo ya mipaka ya nchi hizo ili kujiridhisha na kazi iliyofanywa na wataalamu na kisha kutoka mapendekezo yao kwa mamlaka husika kwa ajili ya kutolewa maamuzi.

Sauti ya Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani balozi Hassan Simba akielezea mikakati ya Serikali ya Tanzania na Uganda