Jumapili , 3rd Jul , 2022

Tembo wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 50 wameweka kambi katika kata ya Mkoka wilayani Nachingwea Mkoani Lindi, wakionekana kutafuta chakula wakitokea porini, jambo lililowafanya wanakijiji wa kata hiyo kukaa macho kwa takribani saa 08 kwa kuhofia usalama wao na mali zao.

Taarifa za awali kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Rweje katani hapo wamesema walishindwa kukadiria idadi ya tembo hao kwakuwa waliweka Nanga kijijini hapo kwenye nyakati za usiku wa saa tano wakitafuta chakula na kupiga kelele nyingi, ambapo asubuhi wamegundua uharibifu uliofanywa na wanyama hao ni pamoja na kula mahindi ambayo hayajavunwa, mtama na korosho.

Tembo hao wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 50 wameonekana katikati ya kijiji cha Rweje na Mkoka mida ya saa moja asubuhi wakiwa wanaelekea porini