Ijumaa , 3rd Jul , 2015

Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania TFDA, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, imetoa mwezi mmoja kwa Wafanyabiashara wa vipodozi kusajili bidhaa wanazoingiza nchini kutoka nchi jirani.

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa-TFDA Kanda ya nyanda za Juu kusini, Analanga Rodney.

Agizo hilo limetolewa na Kaimu Meneja wa amamlaka hiyo ya Nyanda za juu kusini, Analanga Rodney ili kudhibiti uingizwaji wa vipodozi vyenye viambata vya sumu zenye madhara kwa watumiaji.

Rodney amesema wameanza ukaguzi ili kudhibiti uingizaji bidhaa hizo ambazo mara nyingi umekua ukifanywa na wafanyabisahra wasiowaaminifu kutokana na serikali kupiga marufuku matumizi ya vipodozi hivyo nchini.

Amesema Juni mwaka huu walikamata tani 16 zenye vipodozi hivyo vyenye sumu vya thamani ya Milioni 20 katika wilaya ya mbozi, Rungwe,Kyela kwenye malori kutoka nchi njirani kupitia mpaka wa Tanzania na Zambia uliopo Tunduma.