Jumanne , 30th Nov , 2021

Meneja Mradi wa Treni ya SGR Mhandisi Machibya Masanja, amesema kuwa Treni ya umeme itakapoanza haitatumia umeme huu wa kawaida unaokatika mara kwa mara, bali inajengewa mtandao wa umeme unaojitegemea.

Treni ya umeme

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 30, 2021, wakati wa mahojiano maalum na East Africa TV, na kusema kwamba hadi sasa serikali imeshatumia si chini ya bilioni 71 kwa ajili ya ujenzi wa mtandao huo.

"Sasa hivi tunajenga mtandao wa umeme mahususi kwa ajili ya uendeshaji wa Treni, hautaingiliana na matumizi mengine ili kuondoa risk ya umeme kukatika, na mpaka sasa tumetumia si chini ya bilioni 71 kujenga mtandao huo," amesema Mhandisi Masanja.