Alhamisi , 27th Oct , 2016

Ufaulu wa mtihani wa Darasa la Saba umeongezeka kwa asilimia 2.52 kutoka asilimia 67.84 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 70.36 mwaka 2016.

Dkt. Charles Msonde, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani

 

Akitangaza matokeo hayo leo jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dkt. Charles Msonde amesema kuwa Jumla ya watahiniwa 555,291 kati ya 789,479 waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu wamefaulu kujiunga na kidato cha kwanza.

Aidha Dkt . Msonde amesema Jumla ya watahiniwa 238 wamefutiwa matokeo ya mtihani huo kutokana na udanganyifu huku shule 6 waalimu, wamiliki wa shule na wasimamizi wa mitihani wakibainika kufanya udanganyifu na kuwafanyia mtihani wanafunzi.

Amesema katika mtihani huo mwaka huu jumla ya watahiniwa 795,739 wa shule za msingi walisajiliwa kufanya mtihani wakiwemo wasichana 422,864. sawa na asilimia 53.14 na wavulana 372,875 sawa na asilimia 46.86. watahiniwa 789.479 sawa na asilimia 99.21 ya waliosajiliwa walifanya mtihani. wasichana wakiwa 419.932 sawa na asilimia 99.31.wavulana walikuwa 369.547 sawa nasilimia 99.11