Jumanne , 6th Dec , 2022

Idara ya Uhamiaji nchini imemkamata na kumrudisha mara moja nchini kwao raia wa Iran aliyefahamika kwa jina la Hamidrrza Mohammad Abraheh, ambaye amekuwepo nchini kwa zaidi ya miezi sita akidaiwa kuratibu uhalifu wote wa kimataifa ikiwemo ugaidi

Kamishna Uhamiaji na Udhibiti wa Mipaka Samweli Miharane

Kamishna Uhamiaji na Udhibiti wa Mipaka Samweli Miharane, amesema mtu huyo alikuwepo nchini akitumia hati ya kusafiria inayomruhusu kuingia na kuishi nchini Tanzania kwa muda mrefu  inayofahamika kama Multiple Visa ambayo amekuwa akisaidiwa na baadhi ya Watanzania kupata nyaraka hizo za kuishi hapa nchini

Aidha Kamishna Miharane amesema katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Novemba mwaka huu kumekuwepo na wimbi kubwa la kuingia kwa wahamiaji haramu hapa nchini ambapo wahamiaji 18,289 walikamatwa huku mikoa ya Pwani na Tanga ikiongoza kwa kuingia wahamiaji hao 

Katika hatua nyingine Kamishna Miharane amewataka Watanzania kuacha kuwasaidia wahamiaji haramu kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wa nchi na watanzania kwa ujumla.