Jumatatu , 24th Aug , 2015

CHAMA cha Waaandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC) kimefanikiwa kuwakutanisha na kumaliza mvutano uliokuwepo awali juu ya chama gani kimepewa ridhaa ya kusimamisha mgombea ubunge katika jimbo la Mtwara mjini na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Mmoja wa Wenyeviti Wenza wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA ,James Mbatia akiongeza na waandishi wa habari.

Akizungumza kwa niaba ya waandishi wengine, mwandishi na mtangazaji wa Redio Pride ya mkoani Mtwara, Andrew Mtuli, amesema kumekuwa na mazingira magumu kwa waandishi katika kipindi hiki ambacho bado kumekuwa na mvutano juu ya nani aliyepewa jimbo na UKAWA.

Aidha baada ya majadiliano ya pamoja viongozi wote kwa pamoja wamekubali kwa kauli moja kwamba UKAWA bado hawajatoa idhini kwa chama chochote kusimamisha mgombea katika jimbo hilo.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wengine, Uledi Hassan, aliwashukuru waandishi wa habari na uongozi wao kwa kuamua kukutana nao ili kuweza kutafuta muafaka wa jambo hilo.