Jumatatu , 14th Sep , 2015

Chama cha NCCR-Mageuzi Misenyi Mkoani Kegera ambacho kilipewa ridhaa ya kusimamisha mbunge katika jimbo la Nkenge kimeeleza kusikitishwa kwake na kitendo cha vyama washirika wa UKAWA vya CHADEMA na CUF, kusimaisha wagombea ubunge katika jimbo hilo

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi na Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, James Mbatia.

Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa NCCR Mageuzi wilaya ya Misenyi Emanuel Mtengwa wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge wa jimbo la Nkenge kupitia hicho Bi. Angelina Mtwangwa.

Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia chama cha Demokrasia Maendeleo CHADEMA, Ngaile Rugashobya amesema kuwa yeye ndiye ameteuliwa na chama hicho kwa kuwa UKAWA wanataka ushindi na siyo ili mradi mgombea wa umoja huo.

Bi. Angelina jana amezindua kampeni zake katika jimbo hilo na kueleza vipaumbele vyake ni kuboresha maisha ya wana Nkenge lakini wagombea wengine nao wanatarajia kuzindua kampeni zao katika jimbo hilo.