Jumatano , 20th Sep , 2017

Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu imewaachia huru vigogo watatu wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka DART akiwepo Mtendaji Mkuu wa Mradi Asteria Mlambo wenzake baada ya kushtakiwa kwa kuhujumu uchumi,kula njama na kusababisha hasara ya Sh 83.5 milioni

Hukumu hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam katika Mahakama Kuu Kisutu na Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage amesema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 10 wa upande wa mashtaka, vielelezo na ushahidi wa upande wa utetezi ameona upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakabili vigogo hao bila mashaka yoyote.

Mbali na Mlambo wengine walioachiwa huru ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Evodius Katale, Mwanasheria Mkuu wa DART, Francis Kugesha na mkurugenzi wa kampuni ya Yukan, Yuda Mwakatobe.

Katika kesi hiyo ilidaiwa kuwa Septemba Mosi na Oktoba Mosi, mwaka 2013 maeneo ya Kinondoni Dar es Salaam, Mlambo, Katale na Kugesha wakiwa wafanyakazi wa mradi huo, walishindwa kutekeleza majukumu yao vizuri na kuisababishia Serikali hasara ya Sh 83.5 milioni.

 Watumishi hao walikuwa wakituhumiwa kuisababishia Serikali hasara ya mamilioni Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru vigogo watatu wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka(DART), akiwemo mtendaji mkuu wa mradi huo, Asteria Mlambo na mwenzao.