Ijumaa , 22nd Oct , 2021

Machinga zaidi ya 5,000 waliopo katika eneo la Makoroboi jijini Mwanza licha ya kutii agizo la Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Robert Gabriel la kuwataka kupisha katika eneo hilo wamemlilia Rais Samia kwani wamevunja vibanda vyao na hawana eneo mbadala la kufanyia biashara zao.

Mmoja wa machinga akilia mara baada ya kuvunja kibanda chake

Machinga hao ambao walioamua kutii agizo hilo huku wakisema hawajui wapi wanaelekea baada ya maeneo waliyopangiwa kujaa, kilio chao wanakielekeza kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Hapo jan Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Robert Gabriel jana Oktoba 21, 2021, alitoa muda wa saa 24 kwa wafanyabiashara ndogo ndogo wa eneo hilo kuondoka na kwenda kwenye maeneo rasmi waliyotengewa.