Jumanne , 1st Mar , 2016

Wabunge wa mkoa wa Tabora wameitaka serikali kuingilia kati mgogoro wa wakulima na makampuni ya wanunuzi wa tumbaku TLTC na Aliance one ili kuondoa changamoto zinazowakabili wakulima hao.

Wakulima wakiangalia tumbaku ilivyostawi wakati wakiwa hawana uhakika wa bei ya kuridhisha katika mauzo ya Tumbaku hiyo

Wakiongea katika mkutano mkuu wa Chama cha Ushirika wa Tumbaku kanda ya magharibi wabunge hao wamesema kuwa wanunuzi wa tumbaku wamekuwa wakiwalangua wakulima na kurudisha nyuma maendeleo yao.

Wabunge hao wamesema serikali imekuwa ikiwalea sana wanunuzi wa tumbaku na wakulima wakiendelea kunyonywa hivyo haina budi kuchukua hatua za haraka ili kuwanusuru wakulima hao.

Mkoa wa Tabora unazalisha zaidi ya robo tatu ya tumbaku yote inayolimwa nchini Tanzania ingawa inaonesha kuwa wakulima wa zao hilo bado hawajafaidika na zao hilo.