Alhamisi , 7th Jul , 2022

Mbunge wa chama cha Conservative nchini Uingereza Julian Smith amesema  kwenye Kipindi cha Radio 4 mapema leo kwamba wabunge wengi sasa wanataka Johnson ajiuzulu na kudai kuwa nchi hiyo ipo katika mgogoro wa kikatiba, kwani waziri mkuu hana imani na chama chake

Smith amesema kwamba Bw. Borris mwenye mtindo wa Trump na kutishia changamoto ya mfumo wa uongozi hakupaswa kuwa katika Kasri ya Downing Street licha ya kuonekana kutokuwa tayari kuachia kiti hicho mhimu katika utawala wa Uingereza.

Katika Vuta nikuvute hiyo ya kisiasa nchini Uingereza ambayo inamuweka kati Waziri Mkuu Borris Johnson, Katibu wa zamani wa Ireland ya Kaskazini aliyefutwa kazi na waziri mkuu Bw. Borris mnamo Februari 2020, amesema kuwa ni "hoja ya msingi" kwa Boris Johnson kudai ana mamlaka ya kibinafsi ya kutawala.