Alhamisi , 26th Mar , 2015

Wafanyabiasha wa maduka makubwa mkoani Kilimanjaro wamefunga maduka kwa muda usiojulikana kwa madai ya kugomea mashine za kieletroniki (EFD) pamoja na kulalamikia mamlaka ya mapato nchini TRA kuongeza kodi kwa asilimia mia moja.

Wafanyabishara hao wamesema wamelazimika kufunga maduka yao kutokana na kulalamikia mamlaka ya mapato nchini kupandisha kodi kwa asilimia mia moja bila kuwashirikisha, sanjari na kushindwa kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mashine za kielektroniki.

Katibu wa chama cha wafanyabiashara mkoa wa Kilimanjaro Bw. Mmasi Sambuo amesema mpaka sasa wafanyabiashara hawajalipa kodi na kwamba kama serikali haitasikiliza malalamiko ya wafanybishara hao watajiondoa kwenye biashara ikifika Aprili Mosi mwaka huu.

Kwa upande wake meneja wa mamlaka ya mapato nchini tra mkoa wa Kilimanjaro Bw. Abdul Mapembe amesema anasikitishwa na hatua ya wafanyabiashara kufunga maduka kwa kuwa viongozi wa chama hicho walitakiwa kuwasilisha changamoto zinazowakabili wafanyabiashara ili zitafutiwe ufumbuzi kwa mkoa na taifa kwa ujumla