Alhamisi , 5th Mei , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Kegera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu, amesema idadi ya watumishi hewa mkoani humo imeongezeka kutoka watumishi hewa 14 mpaka 99 ambao wanaisababisha serikali hasara zaidi ya shilingi milioni 545.6.

Mkuu wa Mkoa wa Kegera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa watumishi hao hewa wamebainika kutokana na na taarifa ya timu ya uchunguzi ya kubaini watumishi iliyoundwa mkoani humo.

Pia, Meja Jenerali Kijuu, amesema kuna kiasi kidogo cha fedha ambacho wamefanikiwa kukirejesha serikalini lakini hali hiyo ya kusuasa kwa marejesho hayo inatokana na watumishi hewa kutopatikana ingawa bado wanaendelea kuwasaka.

Aidha, Jenerali Kijuu amesema kuwa baada ya kukamilika kwa ukaguzi huo ambao ameuita wa awali itaundwa tume nyingine itakayozunguka kwenye halmashauri na katika kila Kata ili kujiridhisha juu ya taarifa hizo.