Jumatano , 27th Oct , 2021

Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima, amesema kuwa wizara hiyo itawachukulia hatua wale wote watakaobainika kuhusika katika kuvujisha mtihani wa kitaaluma wa mwaka wa pili wa matabibu pindi tu ripoti ya uchunguzi itakapokamilika na kuwasilishwa.

Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima

Waziri Gwajima ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Morogoro na kusema kuwa uchunguzi huo unashirikisha vyombo vyote vya usalama.

"Serikali imeunda kamati ya uchunguzi iliyoshirikisha vyombo vyote, wakiwemo polisi na vyombo vyote vingine vinavyohusika na kuchunguza tuhuma kama hizi, ripoti ipo hatua za mwisho kukamilika, itasomwa wazi, maana wahalifu hao walichokitafuta watakipata", amesema Dkt. Gwajima.

Serikali kupitia Wizara ya Afya itachukua hatua hizo kwa kufuata sheria, kanuni na miongozo bila kuonea yoyote ili iwe fundisho kwa wengine wanaofanya vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na taratibu na sheria  za nchi.