Jumatatu , 6th Jun , 2016

Serikali ya Tanzania imesema kuwa katika kumaliza tatizo la walimu wa sayansi nchini serikali itatoa kipaumbele cha ajira kwa walimu wa masomo hayo lakini pia wataandaa utaratibu maalumu wa kuwarejesha walimu wastaafu wa masomo ya Sayansi.

Naibu wa Wizara ya TAMISEMI, Mhe. Seleman Jaffo

Akizungumza leo Bungeni Mjini Dodoma, katika kipindi cha maswali na majibu, Naibu wa Wizara ya TAMISEMI, Mhe. Seleman Jaffo amesema kuwa pamoja na utaratibu huo lakini pia wataandaa programu maalum ya kuwawezesha mbinu za kiufundishaji wahitimu wa elimu wa masomo ya sayansi ili kuwapa ajira.

Mhe. Jaffo amesema kwa sera ya ujenzi wa maabara kwa kila shule imeongeza changamoto ya hutaji wa walimu wa Sayansi hivyo kwa kufanya hivyo serikali itaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la uhaba wa walimu wa sayansi.

Aidha Mhe. Jaffo ameongeza kuwa serikali imetoa miongozo katika halmashauri zote nchini kuhusu suala la uchangiaji wa ada katika mashule huku ikisisitiza kutoa kipaumbele kwa walimu wa sayansi wanaotafuta ajira.

Sauti ya Naibu wa Wizara ya TAMISEMI, Mhe. Seleman Jaffo