Jumapili , 15th Feb , 2015

Vijana zaidi ya 30,000 waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) nchini Tanzania katika miaka ya 2004 – 2006 wameiomba serikali kuangalia namna watakavyoweza kuwapatia ajira kutokana na kukaa muda mrefu bila ya kuwa na ajira.

Wakizungumza kwa niaba ya vijana hao leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kukusanyika kwa pamoja viongozi wa vijana hao wamesema wamefanya jitihada mbalimbali za kutaka kukutana Rais Jakaya Kikwete kwa lengo la kumueleza matatizo yao lakini wamekuwa wakikumbana na vikwazo vikiwemo vya kuzuiliwa na jeshi la polisi.

Wamesema kwa sasa wanahangaika kutokana na kukosa ajira huku wakiwa na ujuzi wa kutosha kutokana na mafunzo ya kijeshi waliyoyapata hivyo ni vema serikali ikaangalia uwezekano wa kuwapatia ajira vijana hao ili kuepukana na vishawishi vinavyoweza kujitokeza.