Jumatano , 24th Nov , 2021

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru Serikali imeamua kuwarejesha shuleni wanafunzi wote walioacha masomo kwa kupata ujauzito na utoro.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako

Prof. Joyce Ndalichako ameyasema hayo leo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu Mafanikio ya Sekta ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania  leo Novemba 24, 2021 jijini Dodoma.

Aidha Prof. Ndalichako ametangaza kuwa wanafunzi wote 907,802 waliofaulu mtihani wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2022 huku ikisema imawapa kipaumbele wanafunzi wa vijijini katika shule za kitaifa za bweni.

Kwa upande mwingine Prof. Joyce Ndalichako amesema wanafunzi wa darasa la saba wanaofutiwa matokeo kutokana na udanganyifu, wanaoshindwa kufaulu mitihani au wanaopata changamoto zozote wakati wa mitihani yao watapewa fursa ya kurudia mitihani hiyo mwaka unaofuata.