Jumamosi , 27th Aug , 2016

Ukaguzi uliofanywa na Wizara ya Elimu katika shule 6,831 za msingi mwaka 2015/16 umebaini kuwepo kwa wanafunzi 10,273 wasiojuajua kusoma wala kuandika.

Wanafunzi katika moja ya shule za msingi nchini wakiwa darasani

Jambo hilo limeilazimu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kutoa mafunzo kwa wadhibiti ubora wa shule 1,469 ili kuondoa tatizo la wanafunzi wanaomaliza shule wakiwa awajui kusoma wala kuandika.

Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam Jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi wa Idara ya ya udhibiti Ubora wa Shule Bi. Merisela Wasena amesema baada ya kufanya utafiti katika shule za msingi 6,831 wamebaini idadi hiyo ya wanafunzi wasiojua kusoma wala kuandika katika shule 515 huku wasichana wakiwa ni 5, 263 na wavulana ni 5010.

Merisela amesema, hatua ya sasa imechukuliwa kupitia mpango wa ufundishaji na ujifunzaji wa kusoma, kuandika na kuhesabu KKK chini ya mtaala wa shule za msingi kwa darasa la kwanza na darasa la pili litawawezesha wanafunzi kufika darasa la nne wakiwa wanajua kusoma na kuandika hivyo kuondoa changamoto hiyo wafikapo darasa la saba.

Aidha, Merisela amesema wadhibiti ubora wamepewa mafunzo katika maeneo ya Udhibiti wa shule, uchambuzi wa mtaala, Muhtasari, Miongozo ya kufundishia KKK, umahiri wa kusoma, kuandika na kuhesabu.

Maeneo mengine ni pamoja na maandalizi ya ufundishaji upimaji unaozingatia umahiri na kuandaa zana za ufuatiliaji wa utekelezaji wa mtaala wa darasa la kwanza na la pili.