Alhamisi , 26th Nov , 2015

Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi nchini Tanzania imesema Wanafunzi 3045 wa shule za sekondari

Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi nchini Tanzania imesema Wanafunzi 3045 wa shule za sekondari pamoja na wanafunzi wa shule za msingi nchini wameacha shule kutokana na kupata mimba katika mwaka 2013 hali inayochangiwa na umasikini katika ngazi ya familia.

Akizungumza wakati wa uzinduzi maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, mkurugenzi wa shirika la wanawake katika sheria na maendeleo barani Afrika Wildaf nchini Tanzania Judith Odunga, amesema wameyakutanisha mashirika mbalimbali ya kuwatetea wanawake nchini kuzungumzia ukatili kwa wanafunzi wa kike kwa kuhamasisha kupata elimu.

Akizindua siku 16 za kupinga ukatili nchini , mkurugenzi wa elimu ya sekondari mchini, Pauline Mkonongo amesema idadi ya wanafunzi wanaoacha shule kutokana na mimba za utotoni imekuwa ikiongezeka na kukatiza ndoto zao.