Jumanne , 24th Jan , 2023

Zaidi ya wakazi 480000 wa kata tatu za Katwe, Bupandwa na Bangwe zilizopo katika halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza wanatarajiwa kuondokana na changamoto ya kuliwa na mamba pamoja na adha ya kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 15 kutafuta maji

Hii ni baada ya mradi wa maji kujengwa katika Kijiji cha Katwe.

Mradi huo wa maji unaojengwa na kampuni ya Emirates Builders Limited natarajiwa kukamilika mwaka huu ambapo utawasaidia wakazi hao kuwanusuru kuliwa na mamba kama anavyobainisha mbunge wa jimbo hilo la Buchosa Erick Shigongo

‘Nimekulia hapa nimeishi na nyie hapa nashuhudia wazazi wangu wanachota maji umbali mrefu sana ziwani nimeshuhudia wakina mama wakiliwa na mamba naletewa picha za kina mama wakiwa wameliwa na mamba wakiwa wameenda kuchota maji ziwani sasa Rais wetu ametuletea bilioni 15 za miradi yay a maji kuna sababu ya kutomshukuru? Hebu tumshangilie Rias wetu nyinyi ni mashahidi tangu tumepata uhuru wan chi hii hakujawahi kutokea mmwagiko wa pea nyingi kwenye majimbo kama sasa hivi’

Mhandisi Mnyeti Jackson ndiye anayetekeleza mradi huo wa maji kupitia kampuni ya Emirates Builders Limited anaeleza maendeleo ya mradi huo

‘Kwahiyo hapa kwa akzi ambazo tunaendelea nazo sasa hivi ni kule kwenye chanzo kama ulivyoona hapa kwenye matenki tumefikia hatua hii bado fensi na kupaka rangi, na kufunga mabomba na kujenga nyumba ya juu kwahiyo tutakuwa tunasubiria umeme na pampu’