Jumatatu , 22nd Apr , 2024

Serikali imesema wakati wa uchaguzi, Wasimamizi wa uchaguzi na Wasimamizi wasaidizi ngazi ya Jimbo na Kata hulipwa posho za kujikimu wanapotekeleza majukumu ya uchaguzi kwa kuzingatia Waraka wa Utumishi wa Umma kuhusiana na posho za Serikali ambapo imefanya maboresho kwa kuongeza posho.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Angelina Malembeka aliyetaka kujua kuna mpango gani wa kuongeza posho kwa askari na maafisa Wasimamizi wa uchaguzi.

“Kwa upande wa Watendaji na walinzi wa vituo vya kupigia kura utaratibu wa uboreshaji wa viwango vyao vya posho utazingatiwa wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Bajeti ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.” amesema Naibu Waziri Katambi