Jumamosi , 2nd Jul , 2022

Watu watano wamefariki dunia katika ajali ya basi la kampuni ya Sasbosa, ambayo imetokea Julai Mosi, 2022, katika Kijiji cha Mabangwe wilayani Sikonge, ambalo lilikuwa likitokea mkoa wa Mbeya kwenda mkoani Tabora.

Basi lililopata ajali

Chazo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa ni kupasuka kwa tairi ya mbele, na kwamba waliofariki katika ajali hiyo watatu ni wanawake, mwanaume mmoja na mtoto wa mmoja wa kike.

Aidha majeruhi 29 wamelazwa katika hospital teule ya wilaya ya Sikonge, 6 wamepewa rufaa kwa matibu zaidi, 5 wapo hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora  Kitete na mmoja anaendelea na matibabu katika hospitali binafsi ya Malolo.