Jumatano , 23rd Jul , 2014

Wito umetolewa kwa Watanzania kujijengea tabia ya kuwaenzi mashujaa waliojitolea mhanga maisha yao katika ukombozi, kulinda na kujenga taifa la Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Mecky Sadiki.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadik, wakati akielezea maadhimisho ya siku ya mashujaa nchini tarehe 25 mwezi huu Mnazi Mmoja ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais Dk. Jakaya Kikwete.

Bw. Sadick amesema kuwa Maadhimisho hayo yataambatana na gwaride la kumbukumbu litakaloandaliwa na vikosi vya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Jeshi la Magereza pamoja na Jeshi la Polisi.

Amesema siku ya Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mashujaa barabara ya Lumumba, Uhuru na Bibi Titi zitafungwa kwa muda ili kuhakikisha usalama kwa wale wote watakaokuwa wanahudhuria maadhimisho hayo.