Alhamisi , 2nd Dec , 2021

Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Gaudence Milanzi, amewataka Watanzania wanaoishi nchini Afrika Kusini, kuhakikisha wanazingatia maelekezo yanayotolewa na serikali kuhusu kirusi kipya kilichotangazwa nchini humo.

Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Gaudence Milanzi

Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 2, 2021, kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio, wakati akizungumzia hali ilivyo kwa sasa nchini humo tangu Shirika la Afya Dunia (WHO), lilipotangaza uwepo wa kirusi kipya cha Omicron ikiwa ni wimbi la nne la COVID-19.

"Kwa Watanzania wanaoishi nchini Afrika Kusini wao waendelee kusikiliza maelekezo yanayotolewa na serikali, hasa kuhusu kuchukua kinga na tahadhari ya haya maambukizi," amesema Balozi Milanzi.