Jumatatu , 18th Jan , 2016

Waumini wa dini nchini na Watanzania wametakiwa kuiombea Zanzibar ili iendelee kuwa na amani na utulivu kutokana na kukabiliwa na mvutano wa kisiasa baada ya Tume ya Uchaguzi visiwani humo kufuta matokeo ya Uchaguzi na kuamuru urudiwe.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama

Wito huo umetolewa jana mkoani Mtwara na Askofu mkuu wa kanisa Katoliki Jimbo la Mwanza, Mwasham Tadeus Rwaichi, katika sherehe za kumsimika Askofu mkuu wa jimbo katoliki la Mtwara, Mwasham Titus Mdowe, zilizofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki mjini humo na kuhudhuriwa na waumini wa kikristo kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini.

Kwa upande wake, Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Jenister Mhagama, amewataka waumini wa dini kuzidi kuliombea dua taifa la Tanzania chini ya serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ili liendelee kuwa la amani na utulivu kama ilivyokuwa katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka 2015.

Naye, Askofu Titus Mdowe, akizungumza mwishoni baada ya kusimikwa, amewashukuru waumini wote waliohudhuria na kufanikisha kwa sherehe hizo na kuahidi kufanya kazi kwa juhudi zote na kwamba yeye ni kiongozi wa wote hivyo atafanya kazi na kila mtu.