Alhamisi , 8th Oct , 2015

Watanzania wamehimizwa kutumia fursa zilizipo kwa kuwa wabunifu na kufanya tafiti zitakazowasaidia kuwa wawekezaji ili kuongeza ajira na kujiongezea kipato.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyerembe Munasa Sabi akiongea na wadau mbalimbali wa Maendeleo

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyerembe Munasa Sabi amewaambia waandishi wa habari kuwa watanzania walio wengi hawafikirii kuwa wawekezaji na badala yake wamejikita kufanya biashara za kichuuzi ambazo amezitaja kuwa hazina tija.

Amesema kuwa ni vyema wakafanya tafiti kwenye maeneo yao kabla ya kufanya biashara na kuwekeza fedha kwenye bidhaa zao.

Amesema kuwa mkoa wa Mbeya umejaliwa kuwa na fursa nyingi ukiwemo uwanja wa kimataifa wa Songwe, ardhi yenye rutuba nzuri inayokubali mazao mengi na kwamba ni kitovu cha baishara kati ya nchi jirani za Malawi na Zambia hivyo fursa hizo zikitumia ipasavyo zinaweza kuleta tija.