Jumanne , 9th Aug , 2022

Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kufanya mapitio ya mitaala ya elimu ya awali, msingi, sekondari na ualimu ikiwa ni utekelezwaji wa jukumu la msingi la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), ambayo hufanyika kila baada ya mzunguko mmoja wa elimu kukamilika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Anneth Komba

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa TET, Dkt. Anneth Komba, amesema kuwa mabadiliko ya sayansi, teknolojia na uchumi yanapelekea mitaala iliyopo ibadilishwe ili iweze kuendana na mahitaji ya aina ya wahitimu wanaohitajika katika karne hii.

Aidha Dkt. Aneth, amezungumzia utafiti unaofanywa na TET ambao umebaini kuwa watoto wengi hawaelewi wanachofundiahwa, hivyo TET inakuja na tafiti ambayo itawasaidia walimu kufundisha kwa kutumia TEHAMA, jambo litakalosaidia kukuza uelewa kwa wanafunzi.