Watu wawili wafariki dunia wakibatizwa

Monday , 17th Jul , 2017

Watu wawili wamefariki dunia wakati wakibatizwa kwenye mto Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro jana Jumapili.

Naibu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Selemani Issa, watu hao walikuwa wakibatizwa kwa kuzamishwa ndani ya maji, shughuli iliyokuwa ikifanywa na Muhubiri wa Kanisa la Shalom huko Rombo.

 

Watu hao walizama kwenye mto Ugwasi wakati wakizamishwa kwa kile kilichoelezwa na Kamanda Issa kuwa ni kuzidiwa na mawimbi makali ya mto huo.

 

Kwa mujibu wa Kamanda Issa, Polisi wameopoa maiti  na kwamba, baadhi ya waumini wa Kanisa na Mhubiri wanazuiliwa kwa mahojiano zaidi.

 

Recent Posts

Madam Flora

Entertainment
"Sasa sitakaa kimya tena" - Madam Flora

Msanii Beka Flavour

Entertainment
"Simuogopi wala simfikirii Aslay" - Beka Flavour

Matajili wa Alizeti timu ya soka ya Singida United ya Singida wakijifua jijini Mwanza.

Sport
Singida United yasajili 16

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.

Current Affairs
Tiba asili na tiba mbadala wabanwa