Ijumaa , 5th Aug , 2022

Waziri wa maji Jumaa Aweso amesema atawachukulia hatua wakurugenzi wa mabonde ya maji  nchini wanaokaa ofisini na kushindwa kwenda kutoa elimu kwa wananchi juu ya utambuzi na uhifadhi wa vyanzo vya maji ili kusaidia  kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi 

Waziri wa maji Jumaa Aweso

Waziri aweso ametoa onyo hilo baada ya kutembelea chanzo cha maji cha hayuya kilichopo kijiji cha Mwakenjwe Mkoani Mbeya ambapo  amesema ni jambo lakushangaza kuona Mkurugenzi wa bonde anashindwa kujua hata mipaka ya eneo lake ili kuiainisha vyanzo vya maji na kuvihifadhi 

Mhandisi Mbogo Futakamba ni mwenyekiti wa bodi za maji taifa ambapo amewataka wananchi kuendeea kulinda na kutunza vyanzo vya maji kutokana na umuhimu wake.