Jumamosi , 22nd Aug , 2015

Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Fredrick Sumaye ametangaza kujiondoa rasmi katika chama tawala nchini Tanzania CCM na kujiunga na umoja wa katiba ya wananchi UKAWA.

Waziri mkuu msataafu wa awamu ya tatu Mh. Fredrick Sumaye

Mh. Sumaye ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam na wakati akiongea na waandishi wa habari na anakuwa waziri mkuu msaatafu wa pili kujiunga na UKAWA baada Mh. Edward Lowasa kufanya Hivyo.

Mh. Sumaye ambaye hakutaka kutaja chama anachojiunga nacho amesema amekuja kuupa nguvu umoja huo kwa sasa ili kuleta mabadiliko katika nchi ikiwemo mifumo iliypo sasa ambayo inafanya nchi kutokusogea mbele.

Mh. Sumaye amesema kuwa vyama vya upinzani vimejenga misingi imara ya kisera na kuonesha nia ya mabadiliko huku akiwasifu Dk. Slaa na Prof. Lipumba ni moja kati ya waliousimamisha upinzani vyema.

Ameongeza kuwa CCM hawana haja ya kulalamika kwa kuhama kwake kwa kuwa hakuna nafasi yoyote ndani ya chama hicho kwa hiyo anaamini hataathirika sana kutokana na uamuzi wake huo.

Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA unaundwa na vyama vya Chadema, CUF, NCCR Mageuzi pamoja na NLD ambapo mpaka sasa vyama hivyo havijatangaza rasmi siku ya kuanza kampeni.