Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana wilayani Wanging'ombe, wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya uhifadhi katika Pori la Akiba la Mpanga Kipengere.
Waziri Chana ameeleza kuwa jitihada alizofanya na anazoendelea kuzifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za kuitangaza sekta ya utalii kupitia filamu ya Royal Tour ni lazima ziungwe mkono na wadau mbalimbali na Halmashauri zote kwa kuhakikisha zinaweka mazingira mazuri na rafiki kwa watalii.