TAMWA yatoa neno uteuzi wa JPM

Jumatatu , 30th Nov , 2020

Mkurugenzi Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania, (TAMWA), Rose Reuben amesema amefurahishwa na uteuzi uliofanyawa na Rais John Magufuli, kwani umezingatia usawa wa kijinsia.

Mkurugenzi Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania, (TAMWA), Rose Reuben

Bi.Rose ametoa pongezi leo akiwa kwenye mahojiano katika kipindi cha Supa Breakfast, cha  East Africa Radio, ambapo amesema uteuzi wa Rais Magufuli unadhihirisha kuwa yale yote waliyokuwa wanasema kuhusiana na wanawake yalikuwa mambo ya msingi.

"Nimeufurahia uteuzi wa Rais John Magufuli kwasababu umeweza kukumbuka na kuelewa yale tuliyokuwa tukishawishi kwamba  upo umuhimu wa kuwaweka wanawake katika ngazi mbalimbali" amesema Rose Reuben

"Rais Magufuli aliahidi kutekeleza kuhusiana na kuwapatia ngazi za maamuzi wanawake na hivi sisi ameanza kutekeleza kwasababu kati ya wawili aliowateuwa jana moja ni mwanamke na mwingine ni mwanaume hivyo amezingatia usawa wa jinsia" ameongeza Bi.Rose

Aidha Bi Rose amewataka viongozi walioteuliwa kuzingatia misingi ya uongozi kwani wamefika hapo kwa ajili ya kuwatumikia watanzania na nyuma yao yupo mwanamke. hivyo waende wakaendeleza sera zitakazo wasaidia wanawake na kutatua matatizo yao.

Kauli ya Bi Rose inafuatia baada ya uteuzi wa Rais Magufuli siku ya jana ambapo aliwateua Bi. Riziki Said Lulida na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi (CCM),Humphrey Polepole, kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.