Jumamosi , 17th Oct , 2015

Msanii wa muziki wa kimataifa kutoka Nigeria, Wizkid anashikilia rekodi ya kuwa staa wa muziki mwenye rekodi nyingi zaidi ambazo ni maarufu zikiwa zinafikia 50 pembeni ya zile ambazo amezifanya kawaida.

Wizkid

Kwa mujibu wa uchambuzi wa hivi karibuni, kutoka katika orodha hiyo, rekodi 10 kali zaidi za msanii huyo ni pamoja na Ojuelegba, Pakuromo, Azonto, Love My Baby, Don't Dull, Show You The Money, Holla At Your Boy, On Top Your Matter, No Lele pamoja na Tease Me / Bad Guys.

Story kubwa ni kuwa nyota huyu anatarajiwa kutua Dar es Salaam, kwaajili ya onesho kubwa kabisa la Wizkid Live in Dar tarehe 31 mwezi huu, ndani ya viwanja vya Leaders Club, tukio kubwa kabisa la burudani la kihistoria ambalo huna sababu ya kulikosa.